MUNGU ANAKUPENDA!!!

Yohana 3:16
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”
HATUSTAHILI UPENDO WAKE KWA SABABU SISI SOTE TUMEFANYA DHAMBI NA HATUNA HAKI
Warumi 3:10
“Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, hakuna mwenye haki hata mmoja.”
Warumi 3:23
“Kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.”

TUNASTAHILI HUKUMU NA MAUTI
Warumi 5:12
“Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.”
Warumi 6:23
“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti…”
Ufunuo wa Yohana 20:14
“…Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.”

MUNGU ANATUTOLEA KARAMA (ZAWADI), UZIMA WA MILELE, KATIKA KRISTO YESU BWANA WETU
Warumi 5:8
“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.”
Warumi 6:23
“…bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”

UNAWEZA KUWA NA ZAWADI HIYO, UZIMA WA MILELE, KWA NJIA YA KUMWAMINI YESU KAMA MWOKOZI WAKO
Yohana 3:36
“Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.”

ULIITIE JINA LA YESU TU, KWA SABABU HAKUNA NJIA NYINGINE
Warumi 10:13
“…Kila atakayeliitia Jina La Bwana ataokoka.”
Yohana 14:6
“Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”
Ikiwa unaamini ya kwamba:
– Umefanya dhambi,
– Unastahili mauti, yaani ziwa la moto,
– Yesu ameshakufia msalabani,
– Unahitaji kumwamini Yeye tu,
unaweza kuomba kwa mfano kama huu:
“Bwana Yesu, najua kwamba nimefanya dhambi, tafadhali unisamehe; sasa hivi ninakuhitaji uwe mwokozi wangu, ninakuamini Wewe tu, kwa sababu hakuna njia nyingine, uniokoe, katika Jina Lako, Amin.”
